Thursday, October 30, 2014

TANZANIA SASA KUWA KAMA CHINA DARAJA LA DAR ES SALAAM MPAKA ZANZIBAR KUJENGWA.


BAADA ya ndoto ya kuziunganisha pande mbili za katikati ya Jiji la Dar es Salaam na Kigamboni kwa daraja lenye umbali wa meta 680, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) linaangalia uwezekano wa kujenga daraja la kihistoria zaidi litakalounganisha Dar es Salaam na Zanzibar.
Kwa sasa, uongozi wa shirika hilo upo katika mazungumzo na wataalamu mbalimbali ili kuangalia uwezekano wa kujenga daraja hilo katika bandari ya Dar es Salaam kwa upande wa Tanzania Bara na Unguja, kwa upande wa Zanzibar.

Umbali kati ya Dar es Salaam na Zanzibar ni kilometa 73.43, sawa na maili 45.62 hivyo kuwapo kwa mradi huo ni jambo linalowezekana, kwani kuna madaraja marefu zaidi duniani yanayounganisha upande mmoja wa bahari na mwingine.

Kwa sasa, daraja refu kabisa duniani ni lile la Danyang–Kunshan lililopo China ambalo lina umbali wa kilometa 165, sawa na maili 102.4. Daraja hilo lilifunguliwa Juni mwaka 2011.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk Ramadhan Dau wakati alipokuwa akijibu swali la Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Said Mtanda ambaye alitaka kufahamu kama kuna matarajio ya kujenga daraja kubwa zaidi, ikiwezekana la kati ya Dar es Salaam na Zanzibar.

Alisema wapo katika mazungumzo na wataalamu mbalimbali ambapo mazungumzo hayo yakienda sawa, ujenzi wa daraja hilo huenda isiwe ndoto, bali ukweli.

"Hilo wazo lipo mheshimiwa na tayari tumeshaanza mazungumzo ya awali, kwa hiyo hilo wazo lipo na sisi tulilifikiria," alisema Dk Dau.

Kamati hiyo ilifanya ziara katika miradi mikubwa mitatu ya shirika hilo ambayo ni daraja la Kigamboni, ujenzi wa nyumba za Mtoni Kijichi na 'Dege Eco village' ambao una nyumba zaidi ya 7,000.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha ziara hiyo, Mtanda alisema, kamati yake imeridhishwa na miradi hiyo ya NSSF ambayo inaendelea huku akitaka kuongezwa kwa kasi ili watanzania waanze kunufaika na miradi hiyo.

"Muangalie na hilo la ujenzi wa daraja la kutoka Dar es Salaam hadi Zanzibar na mradi wa makazi bora na salama ambao utaweza kubadili taswira ya Jiji la Dar es salaam," alisema.

Alisema kamati yake isingependa kuona changamoto zozote ambazo zinaweza kukwamisha miradi hiyo na kwamba serikali kupitia Wizara ya Ujenzi itaangalia namna ya kuunganisha miundombinu karibu na miradi hiyo.

"Lakini pia tumesikia kuwa serikali inadaiwa na mifuko ya hifadhi, tunashauri serikali kuilipa mifuko hii ili kuifanya kuwa na nguvu na kuweza kuleta maendeleo," alisisitiza Mtanda.

Wednesday, October 29, 2014

WATU KUMI WAFARIKI PAPO HAPO KATIKA AJALI ILIYOTOKEA JIJINI ARUSHA NA KUHUSISHA GARI AINA YA HIACE NA LORY KUGONGANA USO KWA USO


Ajali mbaya imetokea leo majira ya saa kumi na moja jioni huko maeneo ya Madira Arumeru jijini Arusha, iliyohusisha gari la abiria aina ya Hice na Roli lenye tera. Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni hice iliyokuwa ikijaribu kuovatake eneo lisilo salama. Katika ajali hiyo watu kadhaa wamepoteza maisha hususan waliokuwa katika Hice

Tuesday, October 21, 2014

KAMANDA WA VIJANA CCM DODOMA AKABIDHI MIFUKO YA SARUJI KWA SHULE YA SECONDARI HIJRA.

Baadhi ya wazazi wa wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya
Hijra Sekondari wakiwa katika sherehe za mahafari ya kuwaaga.
Mfanyabiashara Haidary Gulamali mbaye pia ni Kamanda wa umoja wa
vijana wa chama cha mapinduzi [UVCCM] mkoa wa Dodoma akifafanua jambo
alipokuwa akiongea na wanafunzi waagwa wa kidato cha nne wa shule ya
Hijra Sekondari wakati wa mahafali yao
Mfanya Bishara maarufu Haidary Gulamali akiwakabidhi uongozi wa
shule ya Sekondari ya Hijra ya mjini Dodoma mifuko ya saluji 50 kwa
ajli ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi, ambapo wanafunzi wa shule hiyo
wamekua wakipata tabu ya mabweni hali ilyoulazimu uongozi shuleni hapo
kuteua baadhi ya madarasa kuwa mabweni.
Mmoja wa wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya hijra
Sekondari akipokea cheti cha kumaliza masomo yake toka kwa kamanda wa
UVCCM Haidary Gulamali.

Monday, October 20, 2014

KAMPUNI YA MABIBO BEER WINES AND SPIRITS LIMITED YASISITIZA UTII WA SHERIA BILA SHURUTI

KAMPUNI ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited yenye haki pekee ya kuagiza na kusambaza kinywaji aina ya Windhoek katika soko la Tanzania imetoa wito kwa wakazi wa mji wa Moshi na vitongoji vyake kuzingatia dhana ya utii wa sheria bila shuruti. 

Wito huo ulitolewa na Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea wa kampuni hiyo, James Rugemalira, jana usiku katika hoteli ya Kilimanjaro Mountain Resort iliyoko katika maeneo ya Marangu, Moshi katika Mkoa wa Kilimanjaro, alipokutana na wadau mbalimbali. 

“Naomba kuwakumbusha kuwa kuna amri ya Mahakama ambayo inazuia mtu yeyote kuingiza na kusambaza Windhoek katika soko hapa nchini bila kuomba na kupata kibali kutoka Mabibo. Amri hii ni halali na inapswa ifuatwe,” Rugemalira alisisitiza. 

Akiwa ameambatana na mawakili wake kutoka nje ya nchi na hapa nchini, Rugemalira alisisitiza kuwa bia aina ya Windhoek inayopaswa kuuzwa katika soko la Tanzania lazima iwe na alama ya MB66 na kwamba inasabazwa na kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited. 

“Hivi sasa tunatumia muda huu kutoa elimu na namna ya kuzingatia sheria bila shuruti. Lakini muda utafika na tutawashughulikia wale wote watakao kiuka amri hii,” alisema. 

Katika hafla hiyo, wageni mablimbali walihudghuria, akiwemo Katibu Mtendaji wa Kata ya Marangu Magharibi, Rose Lyimo. 

Rugemalira aliwaomba wananchi kushirikiana na kampuni yake kwa kununua bia halali iliyolipiwa kodi ili kuweza kupanua soko ambalo litawezesha kampuni yake kuanza kuzalisha aina hiyo ya bia hapa nchini. 

Kwa sasa kampuni ya Mabibo inaagiza bia aina ya Windhoek kutoka Namibia. “Tunategemea kujenga kiwanda hapa nchini cha kuzalisha Windhoek. 

Maeneo ambayo tumeona yanafaa ni pamoja na hapa Moshi. Lakini pia tunaweza kufanya hivyo aidha Tanga au Kagera. Hivyo tushirikiane ili tujenge nchi yetu kwa pamoja na tuepeke kununua bidhaa za magendo,” alisisitiza.
 Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited, James Rugemalira  (kushoto), akigongeana glasi na wakili maarufu wa kampuni hiyo, Michael Ngalo.  
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Benadicta Rugemalira (Kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wageni wake. Kushoto ni Mke wa wakili, Camilo Schutte kutoka Uholanzi, Lize Schutte, Padri wa Kanisa Katoriki Parokia ya Himo, Fabian Nderumaki, Wakili Schutte na wakili kutoka Marekani, Chris Provenzano.
Katibu Mtendaji wa Kata ya Marangu Magharibi,  Rose Lyimo (anayeangalia kamera), akifurahia kinyaji bora cha windhoek na wageni wengine waalikwa.

Wadau mbalimbali wakibadilishana mawazo huku wakipata kinywaji bora cha Windhoek Draught.
Viongozi wa Kampuni ya Mabibo na mawakili kutoka Ulaya na Marekani wakipata maelezo juu ya soko la bia aina ya Windhoek kutoka kwa Meneja Mkuu wa Nymbani Hotels and Resort Mansuetha Michael (hayupo pichani). 
Wadau mbalimbali wakibadilishana mawazo mara baada ya kupata maelezo kutoka kwa uongozi wa kampuni ya Mabibo namna ya kuzingatia sheria bila shuruti
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mabibo,  Benedicta Rugemalira akimwelekeza Meneja Mkuu wa Nyumbani Hotels and Resort Mansuetha Michael namna ya kuitambua bia za Windhoek halali zinazotakiwa kuweko kwenye soko la Tanzania zenye code namba ubavuni MB66 .

Mrembo wa Hoteli ya AMEG Lodge Kilimanjaro,  Miriam Ismail akipeleka vinywaji vya windhoek kwa wateja. 
Mzee Rugemalira akitoa maelezo mafupi juu ya ubora wa bia ya Windhoek. 
Mrembo wa Hoteli ya AMEG Lodge Kilimanjaro, Miriam Isumail (kushoto), akiwa na mrembo mwenzie, Modesta Dennis

Saturday, October 18, 2014

KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA CCM CHAENDELEA MJINI DODOMA LEO.


 Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipanga makabrasha tayari kuendesha kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ambapo masuala ya kujiendesha kiuchumi na mipango ya maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa yanajadiliwa.Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa NEC mjini Dodoma ambapo aliwaeleza juu ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana Oktoba 16, 2014 katika siku ya kwanza ya kikao chake cha siku mbili kinachoendelea mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete imejadili na kupitisha Sera ya CCM ya kujitegemea kimapato na kiuchumi. 

Thursday, October 9, 2014

RASIMU YA KATIBA ILIYOPENDEKEZWA RASMI SASA:RAIS KIKWETE AKABIDHIWA MJINI DODOMA.


Mwenyekiti wa Bunge maalum la katiba Mhe.Samuel Sitta akikabidhi rasimu ya katiba inayopendekezwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho kikwete na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Mohamed Ali Shein, wakati wa sherehe za kukabidhi rasimu hiyo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho kikwete na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Mohamed Ali Shein, kwa pamoja wakikata utepe kuzindua rasmi Rasimu ya Katiba inayopendekezwa baada ya kukabidhiwa rasmi na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sita leo mjini Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho kikwete na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Mohamed Ali Shein, kwa pamoja wakiinua kuonyesha Rasimu ya Katiba inayopendekezwa baada ya kukabidhiwa rasmi na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta na kuizindua leo mjini Dodoma.
Wakifurahi kwa pamoja....

Wednesday, October 8, 2014

TUTAFAKARI NENO LA HEKIMA LA MTU HUYU,MARK JAMES MWANDOSYA.

Kuna uhusiano kubwa sana kati ya mabadiliko ya uchumi kwa maana ya mfumo,na uanzishwaji wa vyombo vya udhibiti,dhana ya udhibiti ilipiga kasi baada ya kuanza zoezi la ubinafsishaji wa sekta ya umma.katika hali ya kawaida vyombo vya udhibiti vingeanzishwa kwanza kabla ya zoezi la ubinafsishaji.na ingekuwa vyema pia zoezi la ubinafsishaji liende sambamba na uanzishaji wa vyombo vya udhibiti.

MARK JAMES MWANDOSYA
Katika kitabu chake cha UDHIBITI WA HUDUMA ZA KIUCHUMI TANZANIA.