Na John Banda, Dodoma
Serekali imewataka wajasiriamali wanaopika na kuuza vitafunwa
kuvitunza kwenye vifungashio vizuri ili kuwa kivutio kwa wateja badala
ya kuviacha vikipigwa na vumbi na kutuliwa na wadudu mbalimbali hali
inayowafanya kukata mitaji kutokana na kukosa soko.
Kauri hiyo ilitolewa hivi karibuni na Naibu Waziri Maendeleo ya jamii,
jinsia na watoto Dkt Pindi Chana alipokuwa akizungumza na wajasirimali
wanaotumia Huduma za Benki ya Wanawake Tanzania [TWB] alipotembelea
vikundi vinavyojihusisha na mikopo katika Benki hiyo mjini Dodoma
Dkt Pindi alisema tabia ya watoa huduma hiyo waliyowengi siyo
waangalifu wanapopika vitafunwa hasa Chapati, Vitumbua, Maandazi na
Bagia ambapo wamekua wakiacha bila hatakufunika hali inayotishia afya
za walaji
Alisema kutokana na hali hiyo walaji huacha kununua bidhaa hiyo hali
inayosababisha wengi wao kushinda juani na vitafunwa hivyo kuhalibika
na kukata mitaji na kusababisha familia zao kuyumba na walio na mikopo
kujikuta wakifunga hata simu kwa hofu ya kupigiwa na maafisa mikopo.
‘’Wajasiriamali wanawake pikeni na kutafuta vifungashio vizuri
vitakavyovutia walaji hali itakayowafanya kuwa na wateja wengi na
kukuza mitaji yenu huku mkizitunza vema familia zenu , siku hizi hata
Mahotel makubwa wanatoa tenda ya kutengenezewa vitafunwa sasa
akikukuta mchafu utakosa fursa na kubaki na imani za kulogwa’’,
alisema Naibu Waziri.
Aidha aliwataka wajasiriamali kutokata tamaa kwa sababu maisha ni
hatua maana wengi huishia njiani kutokana na wanapoanza wanataka kupaa
kimaisha kwa kila walichokihitaji na wanapona wanachelewa huamua
kuacha kwa kisingizio cha biashara hiyo haifai.
Kwa upande wake Ofisa mikopo Mwangalizi wa Benki ya Wanawake Tanzania
[TWB] tawi la Dodoma Digna Damas aliwataka wajasiriamali hao kuwa
waamifu katika mikopo wanayochukua ili waendele kufaidika kwa kukuza
mitaji kutokana na aina yoyote ya biashara wanazofanya ili wakwamuke
kiuchumi.
Naibu waziri huyo alitembelea vikundi vitatu vyenye zaidi ya watu mia
kati ya wajasiriamali 3000 wanaotumia benki hiyo mkoani hapa ambao
mpaka sasa wengi wao wameshafuzu kufikia kukopa 3. Milioni tangu
walipoanza na 200,000 mwaka mmoja uliopita.

Iringa road kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kuongea nao
na kuzichukua changamoto zinazowakabili na kuzifikisha kwa wakubwa.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Dkt Pindi Chana
akiffanua jambo alipokuwa akizungumza na wajasiriamali wanaotumia
kukopa Benki ya wanawake Tanzania [TWB] aliwatembelea hivi karibuni
ili kujua namana wanavyojikwamua kiuchumi kutoka na Benki hiyo
inayoendeshwa na Serekali
No comments:
Post a Comment