Monday, June 30, 2014

MILIONI 319 ZAPATIKANA KATIKA HARAMBEE YA UJENZI WA KANISA KATOLIKI LA MAKONGO JUU JIJINI DAR ES SALAAM

 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka (katikati), akizungumza katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa Katoliki la Makongo Juu  iliyofanyika kanisani hapo Juni 29-2014 jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira, Mrs Rugemalira, Paroko wa Parokia ya Makongo Juu, Joseph Masenge, Mwakilishi wa Mkombozi Commecial Benki, Edina Lupembe na Respius Didace.
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka (Wa pili kulia), akizungumza katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa Katoliki la Makongo Juu  iliyofanyika kanisani hapo Juni 29-2014 jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira, Mrs Rugemalira ambao ni wakazi wa Makongo, Paroko wa Parokia ya Makongo Juu na  Joseph Masenge
 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye sherehe hiyo.
 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye sherehe hiyo.
  Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na Paroko wa Parokia ya Makongo, Joseph Masenge wakiwa katika picha ya pamoja na watoto walioahidi kila mmoja kuchangia sh.100,000 za ujenzi wa kanisa hilo.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika harambee hiyo akiwaongoza wageni waalikwa wakati wa kuchukua chakula

Sunday, June 29, 2014

BAADHI YA ABIRIA DODOMA WASHINDWA KUSAFIRI KUTOKANA NA UHABA WA USAFIRI BAADA YA BUNGE LA BAJETI KUMALIZIKA NA VYUO KUFUNGA

Na John Banda, Dodoma
DODOMA imekumbwa na uhaba wa usafiri wa mabasi ya kwenda mikoani
kutokana na vyuo vikuu na vile vya kawada kufungwa katika kipindi
kimoja hali iliyowasababishia  abiria usumbufu mkubwa ikiwa ni pamoja
na nauri kupanda kinyemela.
Wanafunzi hao hasa wa Vyuo vikuu vya Dodoma [UDOM],  Mtakatifu Yohana,
Mipango na Maendeleo Vijijini [IRDP] na kile cha Biashara [CBE]
ambavyo vina wanafunzi wengi vimefungwa kwa likizo ya miezi mitatu.
Wakiongea na mwandishi wa habari hizi walipokutwa wamezagaa katika
kituo cha mabasi ya kwenda mikoani walisema leo ni siku ya tatu tangu
kuusotea usafiri huo bila mafanikio.
Neema Binamu alisema kutokana na wanafunzi wa vyuo vyote kukutana kwa
pamoja kusaka usafiri imekuwa shida kutokana na Idadi ndogo ya mabasi.
Hali iliyosababisha wenye magari wasiyowaaminifu kupandisha bei
kinyemela mpaka kufikia 30,000 badala ya 17000 na wanapolipa kiasi
hicho huandikiwa nauri ya kawaida tofauti na hapo hakuna
anaesikilizwa.

‘’Kikubwa ni kwa vyombo vinavyohusika na usafirishaji vinatakiwa
kujipanga mapema hasa wakati wa misimu kama hii ambayo vyuo vinafungwa
ili kutuepushia usumbufu ambao hata hatujui kama tutondoka au la’’,
alisema
Kwa upande wao baadhi ya maajenti ambao hawakutaka kuandikwa majina
yao walisema vipindi kama hivi ni vya neema kwao kutokana na siku za
kawaida kura dagaa na sasa watakura kuku takribani wiki nzima.
Nae Mmoja wa askari wa usalama barabarani aliyekuwepo kituoni hapo
alisema yeye si msemaji lakini swala Nauri ya mabasi imegwanyika
katika Madaraja matatu ambapo ni 23,000 lile la kwanza na 17,000 la
tatu.
Na kuhusu upandishwaji nauri kiholela alisema hilo wanalo na
wanawapitia abiria wanaosubili usafiri na kuwapa elimu ili wasilipe
zaidi ya nauri iliyowekwa halali.
Askari polisi anayelinda usalama wa abiria na mali zao katika
kituo cha mabasi yaendayo mikoani akijalibu kutoa maelekezo kwa
wanafunzi wa UDOM waliofika kutafuta usafiri kituoni hapo na kukuta
hali ya usafiri hailidhishi kutokana na uchache wa Mabasi.
Baadhi ya Abiria wakitafakari na mabegi yao baada ya kufika kituo
cha mabasi ya kwenda mikoani na kujikuta wakikosa usafiri kutokana na
uchache wa mabasi ulisababishwa na vyuo vilivyopo mkoani Dodoma
kufungwa kwa wakati mmoja

Wednesday, June 25, 2014

MAUAJI YA KUTISHA ... KIKONGWE AUAWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA WILAYANI KAHAMA, MWALI WAKE AHUSISHWA... SAMAHANI KWA PICHA HIZI



Jinsi Bi Rebeka alivyopigwa shoka kichwani hadi ubongo kutoka nje
Bibi mmoja Mkazi wa mtaa wa Nyahanga, wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, Rebeka Sengasenga (82), ameuawa kwa kukatwa na Shoka kichwani kwa kile kinachohisiwa kuwa ni imani za Kishirikina.

Kwa mujibu wa majirani, tukio hilo limetokea leo majira ya saa tatu asubuhi katika Mtaa wa Nyahanga, wilayani humo, ambapo Marehemu Rebeka alienda nyumbani kwa mtoto wake Bundala Sengasenga alikokuwa ameitwa na mke wa Bundala kusaidia kuanika Dengu.
Muonekano wa Mwili wa Marehemu kwa nje

Mwili wa Marehemu Bi Rebeka ukiondolewa eneo la tukio kupelekwa Mochwar
Imeelezwa kuwa Merehemu Rebeka ambaye alikuwa akiishi kwa mwanae mkubwa Stanley Sengasenga katika mtaa huo alifika kwa Bundala muda huo baada ya kuitwa na Magreth Richard ambaye ni mke wa Bundala kwa ajili ya shughuli hiyo.



Katika maelezo yake Magreth amesema Mama mkwe wake Marehemu Rebeka alifikia sebuleni, na kwamba wakati yeye yuko nje, alimwona mtu ambaye hakuweza kumfahamu akitoka sebuleni hapo na kukimbia ndipo alipoangalia na kumkuta Rebeka ameuawa.

Taarifa za awali zimedai, kabla ya tukio Magreth ambaye kwa sasa anashikiliwa na jeshi la polisi mjini Kahama kwa mahojiano alienda nyumba ya jirani kuazima Shoka, ambalo baadaye limekutwa kwenye shimo la maji taka nyumbani hapo.

Shoka hilo limepatikana baada ya mbinu za kiupelelezi za Jeshi la Polisi kuagiza gari la maji taka kuyavuta maji hayo baada ya majirani kudai hawajaona mtu aliyekimbia na shoka muda huo katika mwelekeo ambao Magreth ameelekeza.
Jeshi la Polisi wilaya ya Kahama limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba Mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Wilaya ya Kahama, huku upelelezi ukiendelea. 

DAR ES SALAAM KUWA BONGE LA JIJI SASA,KUJENGWA MAJENGO YA KISASA NA KIVUTIO CHA WATALII.


Pichani ni Jengo litakalojengwa jijini Dar es salaam na litagharimu Dola za kimarekani milioni 77,kutakuwa na hoteli ya hadhi ya Nyota Tano, Ofisi za Biashara, kutakuwa na Sehemu ya kuegesha magari, jengo hili litatakuwa kivutio kwa Wawekezaji na Utalii.
 Baadhi Malori na Vifaa vingine vya kutendea kazi vikiwa tayari kuahiria ujenzi huu unaanza mara moja baada ya zoezi la uwekaji wa jiwe la msingi kukamilika.

Monday, June 16, 2014

Shirika la Kimataifa la Wakimbizi [ IO M] lawafunda waandishi wa Dodoma jinsi ya kuandika habari za wakimbizi


Meneja wa shirika la Kimataifa la Uhamiaji [I O M] Charles Mkude
akiwaonyesha wandishi wa Habari hawapo pichani moja ya picha
zinazoonyesha wakimbizi wanavyosafili kwa tabu kwa kutumia malori,
Meri na maboti wakiwa wamejazana bila kujali watoto na mizigo

Mmoja wa waandishi hao Paul Mabeja akiwasilisha mapendekzo ya
majadiliano ya vikundi kwenye semina hiyo.
Waandishi wa Dodoma wakiwa darasani kwenye mafunzo hayo