Siyo
rahisi kwa mtu ambaye anapata chakula kutwa mara tatu, kuamini kuwa kuna
binadamu ambao wanaweza kuishi hata siku tatu bila kupata hata mlo
mmoja.
Hata
hivyo ni ukweli usiopingika kuwa wakati unakula na kumwaga chakula
kwenye mifuko ya takataka, wapo ambao hutamani kukimbilia mifuko hiyo na
kujitafutia chochote kwa ajili ya matumbo yao.(Martha Magessa)
Wapo
ambao hudiriki kula hata vitu ambavyo havistahili kuliwa na binadamu,
lakini hawana jinsi wanafanya hivyo kutuliza matumbo yao yanayosumbuliwa
na njaa.
Njaa
imekuwa ni tatizo sugu linaloonekana kujitokeza katika mataifa
mbalimbali yanayoendelea, huku bara la Afrika likiwa limeathirika kwa
sehemu kubwa kutokana na janga hili.
Licha ya
kuwa na eneo kubwa la ardhi yenye rutuba na mvua za kutosha, ukanda wa
Afrika Mashariki nao umekuwa ukikumbwa na baa hili katika baadhi ya
maeneo.
Hilo
linatokana na maeneo hayo kuwa na ukame na kukosa mvua, hali
inayopelekea kilimo kutofanyika kama inavyostahili hivyo chakula kuwa
miongoni mwa vitu hadimu kupatika kwa wakazi wa eneo husika.
Kijiji
cha Kakoghit kilichopo kwenye Kata ya Lokis nchini Kenya, kimekuwa
miongoni mwa maeneo ambayo yapo katika hali mbaya zaidi kutokana na
tatizo la njaa.
Tukio la
hivi karibu la familia moja kuchinja paka na kumla kama kitoweo baada ya
kuzidiwa na njaa waliyokaa nayo kwa siku kadhaa kutokana na kukosa
chakula, limedhihirisha namna gani njaa ilivyokuwa tishio.
Familia
hiyo yenye jumla ya watu watatu ikiwajumuisha Jepoterit Yaranyang (80),
Jepteker Ng'uriawing (35) na mtoto wake wa miaka miwili ilifikia uamuzi
wa kumuiba paka wa jirani na kumchinja ili kutuliza njaa iliyokuwa
ikiwasumbua kwa muda mrefu.
Katika
mahojiano yake na gazeti la moja nchini Kenya, Ng'uriawing anasema kuwa
baada ya kukaa siku nyingi bila kula huku mama yake akiwa hoi kitandani
akidhoofika kutokana na njaa, akafikiria kumkamata paka wa jirani ili
wamfanye kitoweo. Wazo hilo likatawala kichwani mwake na dakika chache
alipokatiza paka huyo alimpiga kichwani kabla ya kumchinja na kuchoma
nyama yake kuitafuna ili kupoza njaa iliyokuwa ikiwakabili.
"Baada ya
kuona hali inazidi kuwa mbaya nikaona tutaangamia kwa kuwa mama yangu
tayari alishaanza kudhoofika kutoka na njaa, nikaamua kumgonga paka
kisha nikamchuna ngozi na kuchoma nyama yake ambayo ilikuwa na damu
nyingi"anasema Ng'uriawing na kuongeza:
"Ukweli
ni kwamba hali ilikuwa mbaya sana hata kama paka asingejitokeza
ingewezekana ningemchinja mtoto wangu tuile nyama yake maana nisingeweza
kuvumilia hali ya njaa kali kiasi kile"
No comments:
Post a Comment