Tuesday, November 4, 2014

RAIS KIKWETE AZUNGUMZA NA WAZEE WA MKOA WA DODOMA.


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wazee wa mji wa Dodoma leo Oktoba 11, 2014 waliouitisha ili kuzungumza naye maswala kadhaa ya maendeleo.
 Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani wakati wa  Mazungumzo kati ya RaisJakaya Mrisho Kikwete na  wazee wa mji wa Dodoma leo Oktoba 11, 2014 waliouitisha ili kuzungumza naye maswala kadhaa ya maendeleo.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea risala toka kwa Mwenyekiti wa Wazee wa Mkoa wa Dodoma Balozi Job Lusinde wakati wa mkutano na  wazee wa mji wa Dodoma leo Oktoba 11, 2014 waliouitisha ili kuzungumza naye maswala kadhaa ya maendeleo.
Viongozi wakisimama kuimba  Wimbo wa Taifa
 Ngoma ya utamaduni ya kabila la Wagogo likitumbuiza kabla ya kuanza kwa mkutano wa Rais Kikwete na wazee wa mji wa Dodoma leo Oktoba 11, 2014 waliouitisha ili kuzungumza naye maswala kadhaa ya maendeleo.
  Ngoma ya utamaduni ya kabila la Wagogo likitumbuiza kabla ya kuanza kwa mkutano wa Rais Kikwete na wazee wa mji wa Dodoma leo Oktoba 11, 2014 waliouitisha ili kuzungumza naye maswala kadhaa ya maendeleo.
 Sehemu ya wazee wakati wa  mkutano wao na  Rais Kikwete mjini Dodoma leo Oktoba 11, 2014 waliouitisha ili kuzungumza naye maswala kadhaa ya maendeleo.
 Meza kuu ikiomba dua kabla ya kuanza kwa mkutano wa Rais Kikwete na wazee wa mji wa Dodoma leo Oktoba 11, 2014 waliouitisha ili kuzungumza naye maswala kadhaa ya maendeleo.
 Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali akiingia katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani jijini Dodoma leo Oktoba 11, 2014  tayari kwa mkutano wake na wazee wa mji wa Dodoma leo Oktoba 11, 2014 waliouitisha ili kuzungumza na Rais Kikwete  maswala kadhaa ya maendeleo.
Rais Kikwete akiingia katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani jijini Dodoma leo Oktoba 11, 2014  tayari kwa  mkutano wake na wazee wa mji wa Dodoma leo Oktoba 11, 2014 waliouitisha ili kuzungumza naye masuala kadhaa ya maendeleo. 
Rais Kikwete akiingia katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani jijini Dodoma leo Oktoba 11, 2014  tayari kwa  mkutano wake na wazee wa mji wa Dodoma leo Oktoba 11, 2014 waliouitisha ili kuzungumza naye masuala kadhaa ya maendeleo

Monday, November 3, 2014

HIZI NDIZO VURUGU NDANI YA MDAHALO WA KATIBA.


Jaji Joseph Warioba akitoa mada. 
Mtoa mada katika mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa, Jaji Joseph Warioba akitoa mada kabla ya mkutano huo kuvunjika katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Saam leo.
Baadhi ya vijana walioingia na mabango ndani ya ukumbi wa mkutano wakiwa na mabango yaliyokuwa yakisomeka ‘Katiba inayopendekezwa tumeipokea tunaiunga mkono’.
Mlinzi wa Jaji Joseph Warioba (kushoto) akimkinga kwa mikono ili asipate madhara baada ya mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa kuvamiwa na kundi la vijana na kusababisha uvunjifu wa amani. 
Jaji Joseph Warioba akiangalia usalama wake kabla ya kuondolewa mlinzi wake katika ukumbi wa Ubungo Plaza ambapo mdahalo wa kuijadili Katiba inayopendekezwa ulikuwa ukifanyika kabla ya kuvunjika.
Aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Humphrey Polepole akimzuia mmoja wa vijana aliyekuwa na jazba mara baada ya kutokea kwa vurugu katika mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekeza.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), Joseph Butiku (katikati) akisindikizwa kuingia katika chumba cha VIP mara baada ya kuvunjika kwa mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa. Mdahalo huo uliandalia na taasisi hiyo.
 Vijana wakiwa na mabango. 
 Mabango yakiwa juu. 
 Mmoja wa vijana waliokuwa wakitoa maneno ya kashfa kwa Jaji Warioba akiwanyooshea vidole viongozi wa meza Kuu. 
 Baadhi ya viti vilivyovujwa. 
 Jaji Warioba akitoka katika ukumbi huku akisindikizwa na askari kanzu. 
 Jaji Warioba akisindikizwa na makachero wa Polisi. 
 Jaji Warioba akiwapungia mkono wananchi waliokuwa wamefurika nje ya jengo la Ubungo Plaza ambako mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa ulikuwa ukifanyika.Wananchi walikuwa nje ya jengo la Ubungo Plaza wakimshangilia Jaji Warioba wakati akitoka katika ukumbi wa mdahalo huku wakimuita 'Rais Rais'.(Picha zote na Francis Dande).

Thursday, October 30, 2014

TANZANIA SASA KUWA KAMA CHINA DARAJA LA DAR ES SALAAM MPAKA ZANZIBAR KUJENGWA.


BAADA ya ndoto ya kuziunganisha pande mbili za katikati ya Jiji la Dar es Salaam na Kigamboni kwa daraja lenye umbali wa meta 680, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) linaangalia uwezekano wa kujenga daraja la kihistoria zaidi litakalounganisha Dar es Salaam na Zanzibar.
Kwa sasa, uongozi wa shirika hilo upo katika mazungumzo na wataalamu mbalimbali ili kuangalia uwezekano wa kujenga daraja hilo katika bandari ya Dar es Salaam kwa upande wa Tanzania Bara na Unguja, kwa upande wa Zanzibar.

Umbali kati ya Dar es Salaam na Zanzibar ni kilometa 73.43, sawa na maili 45.62 hivyo kuwapo kwa mradi huo ni jambo linalowezekana, kwani kuna madaraja marefu zaidi duniani yanayounganisha upande mmoja wa bahari na mwingine.

Kwa sasa, daraja refu kabisa duniani ni lile la Danyang–Kunshan lililopo China ambalo lina umbali wa kilometa 165, sawa na maili 102.4. Daraja hilo lilifunguliwa Juni mwaka 2011.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk Ramadhan Dau wakati alipokuwa akijibu swali la Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Said Mtanda ambaye alitaka kufahamu kama kuna matarajio ya kujenga daraja kubwa zaidi, ikiwezekana la kati ya Dar es Salaam na Zanzibar.

Alisema wapo katika mazungumzo na wataalamu mbalimbali ambapo mazungumzo hayo yakienda sawa, ujenzi wa daraja hilo huenda isiwe ndoto, bali ukweli.

"Hilo wazo lipo mheshimiwa na tayari tumeshaanza mazungumzo ya awali, kwa hiyo hilo wazo lipo na sisi tulilifikiria," alisema Dk Dau.

Kamati hiyo ilifanya ziara katika miradi mikubwa mitatu ya shirika hilo ambayo ni daraja la Kigamboni, ujenzi wa nyumba za Mtoni Kijichi na 'Dege Eco village' ambao una nyumba zaidi ya 7,000.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha ziara hiyo, Mtanda alisema, kamati yake imeridhishwa na miradi hiyo ya NSSF ambayo inaendelea huku akitaka kuongezwa kwa kasi ili watanzania waanze kunufaika na miradi hiyo.

"Muangalie na hilo la ujenzi wa daraja la kutoka Dar es Salaam hadi Zanzibar na mradi wa makazi bora na salama ambao utaweza kubadili taswira ya Jiji la Dar es salaam," alisema.

Alisema kamati yake isingependa kuona changamoto zozote ambazo zinaweza kukwamisha miradi hiyo na kwamba serikali kupitia Wizara ya Ujenzi itaangalia namna ya kuunganisha miundombinu karibu na miradi hiyo.

"Lakini pia tumesikia kuwa serikali inadaiwa na mifuko ya hifadhi, tunashauri serikali kuilipa mifuko hii ili kuifanya kuwa na nguvu na kuweza kuleta maendeleo," alisisitiza Mtanda.

Wednesday, October 29, 2014

WATU KUMI WAFARIKI PAPO HAPO KATIKA AJALI ILIYOTOKEA JIJINI ARUSHA NA KUHUSISHA GARI AINA YA HIACE NA LORY KUGONGANA USO KWA USO


Ajali mbaya imetokea leo majira ya saa kumi na moja jioni huko maeneo ya Madira Arumeru jijini Arusha, iliyohusisha gari la abiria aina ya Hice na Roli lenye tera. Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni hice iliyokuwa ikijaribu kuovatake eneo lisilo salama. Katika ajali hiyo watu kadhaa wamepoteza maisha hususan waliokuwa katika Hice

Tuesday, October 21, 2014

KAMANDA WA VIJANA CCM DODOMA AKABIDHI MIFUKO YA SARUJI KWA SHULE YA SECONDARI HIJRA.

Baadhi ya wazazi wa wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya
Hijra Sekondari wakiwa katika sherehe za mahafari ya kuwaaga.
Mfanyabiashara Haidary Gulamali mbaye pia ni Kamanda wa umoja wa
vijana wa chama cha mapinduzi [UVCCM] mkoa wa Dodoma akifafanua jambo
alipokuwa akiongea na wanafunzi waagwa wa kidato cha nne wa shule ya
Hijra Sekondari wakati wa mahafali yao
Mfanya Bishara maarufu Haidary Gulamali akiwakabidhi uongozi wa
shule ya Sekondari ya Hijra ya mjini Dodoma mifuko ya saluji 50 kwa
ajli ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi, ambapo wanafunzi wa shule hiyo
wamekua wakipata tabu ya mabweni hali ilyoulazimu uongozi shuleni hapo
kuteua baadhi ya madarasa kuwa mabweni.
Mmoja wa wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya hijra
Sekondari akipokea cheti cha kumaliza masomo yake toka kwa kamanda wa
UVCCM Haidary Gulamali.