Thursday, January 24, 2013

USIKU WA TARANGIRE WAFANA VILIVYO

Wanamuziki wa Bendi ya FM Academia wakionesha vitu vyao wakati wa Hafla ya usiku wa Tarangire iliyofanyika kwenye hifadhi hiyo ya Taifa.
Mkuu wa Mkoa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (mwenye kilemba/miwani), Mkuu wa Mkoa Manyara Elaston Mbwilo (kulia kwa Dr. Nchimbi) Uongozi na wafanyakazi wa Hifadhi ya Taifa Tarangire wakiserebuka kwa muziki wa Bendi ya FM Academia wakati wa hafla ya Usiku wa Tarangire iliyofanyika hifadhini hapo
Mwanamuziki wa Bendi ya FM Academia Nyoshi El – Saadat (katikati) akifungua Champaign kwenye hafla ya Usiku wa Tarangire iliyofanyika hifadhini hapo ambapo Bendi hiyo FM Academia ilitumbuiza na pia iliimba kibao maalumu kinachohamasisha utalii wa ndani kwa watanzania.

Monday, January 21, 2013

UKUTA WA KITUO CHA MABASI CHA UBUNGO WAANGUKA NA KUHARIBU MAGARI ZAIDI YA 20

 Baadhi ya magari yaliyoangukiwa na ukuta.
 Magari mbalimbali yakiwa chini ya kifusi.
 Gari aina ya Noah likiwa limegandamizwa na zege.
 Hii ndiyo hali halisi ya tukio lilivyokuwa.
 Gari aina ya Toyota likiwa limebonyezwa na zege.
 Watu wakiangalia magari yao.
 Kenyela akiongea jambo juu ya ajali hiyo.
 likuwa ni hasara tupu.
.UKUTA WA ENEO  LA NDANI YA KITUO CHA MABASI UBUNGO BUS TERMINAL UMEANGUKIA MAGARI ZAIDI YA 24 YALIYOKUWA YAMEPAKI ENEO AMBALO HUTUMIKA KUPAKI WAKIWA WANASINDIKIZA ABIRIA NA NDUGU ZAO,CHANZO CHA AJALI HIYO NI MKANDARASI WA ENEO HILO ALIKUWA ANABOMOA UKUTA HUO,NA PIA IMERIPOTIWA KUWA KUNA BAADHI YA MAJERUHI

WOMEN'S DAY 2013

mambo yameiva hayao.

Mh. Lowassa ahudhuria msiba wa mume wa Mbunge wa zamani wa Temeke, Mama Khadija Kusaga

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akimpa pole mfiwa,Mama Khadija Kusaga wakati alipofika nyumbani kwake Keko Maghorofani jijini Dar es salaam jana.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwa katika mazungumzo na Mbunge wa Jimbo la Temeke, Mh. Abbas Mtemvu wakati walipokuwa kwenye msiba huo jana jioni.

YALIYOJIRI MKUTANO MKUU WA MWAKA WA YANGA JANA, SENDEU, MWESIGWA WAFUTIWA UANACHAMA


Mwenyekiti Mpya wa Club ya Yanga Africans, Yusuf Manji akifafanua baadhi ya mambo mbalimbali kwenye mkutano huo,uliochanganua mambo mbalimbali zikiwemo changamoto za timu hiyo, maendeleo ya Klabu hiyo pamoja na ujenzi wa kiwanja kikubwa cha mpira maeneo ya Jangwani,jijini dar, Sahihisho la katiba yao, masuala mbalimbali yanayohusiana na wanachama wao, ustawi wa wanachama wao, mikataba baina yao na wadhamini wao na mambo mengine mengi yaliyoongelewa.
 Sehemu ya meza kuu ya mkutano huo ilivyokuwa.
 Makamu mwenyekiti wa timu ya Yanga,Clement Sanga akitolea ufafanuzi moja ya jambo lililoulizwa na wajumbe wa mkutano huo.
Beki mahiri wa Yanga, Shadrack Nsajigwa (kulia)  akipeana mkono wa shukrani na Mwenyekiti wa Yanga,Yusuf Manji mara baada ya kutajwa kuwa ndiye mchezaji aliyedumu Yanga kwa muda mrefu miongoni mwa wachezaji waliopo hivi sasa, na kuwa mchezaji mwenye nidhamu zaidi, hivyo alizawadiwa barua ya shukurani na kitita cha shilingi milioni moja.

Pichani juu na chini ni baadhi ya Wajumbe wa timu ya Yanga waliopata nafasi ya kuuliza maswali mbalimbali kwa Kamati ya Utendaji,mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria mkutano huo.
 Mwenyekiti wa Yanga,Yusuf Manji sambamba na Makamu mwenyekiti wa timu hiyo,Clement Sanga wakifatilia jambo kwa  makini ukumbini humo.
 Baadhi ya wachezaji wa timu ya Yanga pia walihudhuria mkutano huo uliohusu mikakati mbalimbali ya kuimarisha timu hiyo.
 Baadhi ya Wazee wa baraza wa timu ya Yanga wakifautilia kwa makini yaliyokuwa yakijili kwenye mkutano huo mkuu wa Kihistoria.
 Kocha mpya wa timu ya Yanga,kutoka nchini Uholanzi Ernest Brandts nae aliruhusiwa kutoa yake machache kuhusina na timu yake ya Yanga.
 Baadhi ya Wanachama wa Yanga waliofurika kwa wingi ndani ya mkutano mkuu wa timu hiyo uliofanyika ndani ya bwalo la Maofisa wa Polisi,Oysterbay jijini Dar es salaam mapema leo asubuhi na kumalizika mapema jioni ya leo. 
 Msanii mahiri wa kizazi kipya, Barnaba, pamoja na wasanii wenzake kutoka THT wakitumbuiza kwenye mkutano huo.
Mtangazaji machachari wa kipindi cha michezo,Clouds FM/TV Mbwiga Mbwiguke, akiwaweka sawa wanachama wa Yanga waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wao mkuu wa Mwaka.

RAIS KIKWETE AWASILI UFARANSA

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mke wa Rais wa Mali MamaTouré Lobbo Traoré waliyekutana naye uwanja wa ndege wa Kimataifa Charles de Gaulle jijini Paris, Ufaransa, baada ya kuwasili tayari kuanza ziara ya kiserikali ya siku tatu.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwa na mke wa Rais wa Mali Mama Touré Lobbo Traoré waliyekutana naye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Charles de Gaulle jijini Paris, Ufaransa, baad ya kuwasili tayari kuanza ziara ya kiserikali ya siku tatu.