Monday, January 12, 2015

PICHA MBALIMBALI ZA MATUKIO YA SHEREHE ZA KUMBUKUMBU YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR.


 Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia Mkono wananchi wakati alipowasili katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja katika kilele cha Sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyofanyika leo.
 Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akikagua gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama leo wakati wa  Sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar akifuatana na Paredi Kamanda Luteni kanali Mohamed Khamis Adam  katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika leo katikauwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
 Wananchi mbali mbali waliohudhuria katika sherehe za kilele cha miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar wakimasikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake leo katika kilele hicho Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
 Wafanyakazi wa Ofisi ya rais Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ wakipita mbele ya jukwaa kwa maandamano wakati wa sherehe za Kuadhimisha miaka 51 ya mapinduzi ya Zanzinar akiwa mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.
 Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na baadhi ya viongozi wakati akiwasili uwanjani hapo.
 Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamini Mkapa
 Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif.
 Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi.
 Rais Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Mkuu wa majeshi....
 Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dkt. Shein wakati akiwasili uwanjani hapo na baada ya kukagua gwaride la heshima.
Rais Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Rais wa Zanzibar, Dkt. Shein.

Tuesday, January 6, 2015

POLISI WAFYATUA MABOMU KUZIMA VURUGU WAKATI WA ZOEZI LA KUAPISHWA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA UBUNGO JIJINI DAR ES SALAAM


Polisi Jijini Dar es Salaam wamelazimika kufyatua risasi hewani na kufyatua mabomu ya machozi kufuatia kuibuka kwa vurugu katika hoteli ya Land Mark ambapo shughuli ya uapishaji wa wenyeviti wa serikali Mitaa zinafanyika.
Vurugu hizo, zimeibuliwa na kambi ya upinzani ambayo imelalamikia kuwa Mwenyekiti mmoja wa Chama tawala CCM aliyeapishwa hakuwa ameshinda katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, uliofanyika mwaka jana.

Monday, January 5, 2015

MH RAIS KIKWETE AMWAPISHA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akimwapisha George Mcheche, kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo mchana.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akisaini nyaraka wakati wa hafla fupi ya kumwapisha, George Mcheche, kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kwenye hafla hiyo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo mchana. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akimkabidhi nyaraka za Serikali, George Mcheche, baada ya kumwapisha kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo mchana.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa kwanza kutoka kulia) Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Spika wa Bunge la Jamhuri, Anne Makindajaji Mkuu, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othuman, Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Mcheche, aliyeteuliwa, wakiwa katia ukumbi wakisubiri zoezi hilo la kuapishwa.
 Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliyekuwa akisubiri kuapishwa, George Mcheche, akizungumza jambo na viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, wakati wa hafl hiyo.
 Baadhi ya viongozi waliohudhuria hafla hiyo
 Picha ya pamoja ya kumbukumbu na viongozi wa ngazi za juu.
  Picha ya pamoja ya kumbukumbu na wakuu wa Ulinzi na usalama.
 Picha ya pamoja ya kumbukumbu na wanafamilia wa Bw. George.
 Picha ya pamoja ya kumbukumbu na baadhi ya wafanyakazi wenzake.
Picha ya pamoja ya kumbukumbu na baadhi ya wafanyakazi Tume ya Sheria

Friday, January 2, 2015

WALIOTEMBEA KUTOKA GEITA HADI DAR KUMWONA RAIS WAFIKIA MIKONONI MWA POLISI NA KUWEKWA SELO BADALA YA KUFIKIA IKULU

Vijana watatu wa CHADEMA waliotembea kwa miguu kutoka Geita hadi Dar es Salaam kumwona Rais wamewasili jijini Dar es Salaam leo.
Vijana hao walitaka kumwona Rais ili kuwasilisha ujumbe wao ikiwemo kutoridhishwa na kukithiri kwa vitendo vya kifisadi.
Hata hivyo vijana hao wamezuiwa kumwona Rais kutokana na kutokufuata taratibu za kumwona Rais ikiwa ni pamoja na kutokuomba vibali husika.
Akieleza maamuzi hayo Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana alisema "Kuna utaratibu wa kumwona Rais uliotakiwa kufuatwa. Pia kama wametembea kutoka Geita bila vibali husika basi wamefanya kosa la kisheria."

PANYA ROAD WALETA BALAA DAR ES SALAAM.


Habari zilizotufikia muda huu zinasema kuwa vijana hatari kwa matukio ya unyang'anyi maarufu kama Panya Road, wamevamia maeneo ya Ubungo na Sinza muda huu, ambapo hadi sasa askari wapo eneo la tukio sinza wadhibiti matukio yanayojaribu kufanywa na wa vijana hao huku mabomu ya machozi yakirindima pande hizo. Wadau si vyema kwa muda huu kukatiza anga hizo kuweni makini

Thursday, January 1, 2015

HAPPY NEW YEAR 2015.


KARIBU MWAKA 2015:

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongoza Viongozi na Wananchi kupeperusha bendera ya Taifa wakati ulipoingia mwaka mpya wa 2015 kwenye Tamasha la mkesha na Dua maalum ya kuombea Taifa lililofanyika Uwanja wa Taifa jijini   Dar es salaam jana usiku Disemba 31, 2014/2015.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongoza Viongozi na Wananchi kupeperusha bendera ya Taifa wakati ulipoingia mwaka mpya wa 2015 kwenye Tamasha la mkesha na Dua maalum ya kuombea Taifa lililofanyika Uwanja wa Taifa jijini   Dar es salaam jana usiku Disemba 31, 2014/2015.
 Wananchi mbalimbali wa mkoa wa Dar es salaam wakishangilia kwa furaha wakati Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipokua akihutubia Taifa kwenye Tamasha la Mkesha wa mwaka mpya wa 2015 iliyofanyika Disemba 31, 2014/2015 usiku wa kuamkia mwaka mpya Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na wananchi alipowasili Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jana usiku Disemba 31, 2014/2015 kwa ajili ya kuhudhuria Tamasha la mkesha wa Mwaka Mpya na Dua maalum ya kuliombea Taifa.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia Taifa kwenye Tamasha la Mkesha wa mwaka mpya wa 2015 iliyofanyika Disemba 31, 2014/2015 usiku wa kuamkia mwaka mpya Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwatakia heri ya mwaka mpya wa 2015 Viongozi na Wananchi baada ya kumalizika kwa Tamasha na Dua maalum ya kuliombea Taifa lililofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam  Disemba 31, 214/2015.