Sunday, January 5, 2014

RAIS KIKWETE AONGOZA MAELFU YA WANANCHI KATIKA KUUGA MWILI WA ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA DR WILLIAM MGIMWA KATIKA VIWANJA VYA KARIMJEE JIJINI DAR ES SALAAM.

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete
akiambatana na familia yake wakati alipokuwa akiuaga na kutoa salamu
za mwisho kwa mwili wa marehemu Dr William Mgimwa aliyekuwa waziri wa
Fedha katika viwanja vya karimjee jana.

Makamanda mbalimbali wakiwa katika viwanja vya katimjee kwaajili ya
kuuaga mwili wa maremu Dr. William Mgimwa aliyefariki nchini africa ya
kusini siku ya kwanza ya mwaka huu ambao unatarijawa kufanyiwa ibada
maarumu na kuzikwa kijijini kwao kalenga mkoani iringa

Mke wa hayati Baba wa Taifa Maria Nyerere akiwasili katika viwanja
vya karimjee alipofika kutoa heshima ya mwisho kwa mwili wa marehemu
Dkt William Mgimwa ulioagwa leo jijini Dar es salaam .


Kiongozi wa kambi ya upinzani Freeman Mbowe akitoa salamu za rambirambi.


Mwigulu Nchemba akiongea jambo viwanjani hapo
Mwakilishi wa familia God Mgimwa akitoa shukurani
Baadhi ya watu wakiuaga mwili wa marehemu Mgimwa.
 PICHA NA JOHN BANDA

MHUBIRI WA INJILI AFARIKI DUNIA AKIJARIBU KUTEMBEA JUU YA MAJI KAMA YESU.

Ilikuwa sikitisho kubwa kwa waumini baada ya mchungaji wao kusombwa na maji baada ya kujaribu kutembea juu ya maji kama vile masihi Yesu alivyofanya wakati wake alipokuwa duniani.

Pastor Frank Kabele mwenye umri wa miaka 35, aliwaambia waumini wake kuwa mtu mwenye imani anaweza kufanya miujiza yeyote ila tu uwe na imani. Aliwaahidi wafuasi wake kuwa atatembea juu ya maji pindi tu atakapomaliza maombi yake.

Lakini mambo yalienda ndivyo sivyo baada ya pastor huyo kujaribu kutembea katika mto mkubwa, alididimia mtoni humo na ilikuwa vigumu kwa waumini wake kumsaidia kwani maji yalikuwa na nguvu nyingi

RC DODOMA AWASISITIZA WALEMAVU KUANZISHA MIRADI YA UFUGAJI NYUKI KUPATA KIPATO CHA KUENDESHEA SHUGHULI ZA CHAMA CHAO NA KUJIKIMU.

Mkuu wa mkoa Dodoma Dr Rehema Nchimbi ameziagiza wilaya zote za mkoa wa Dodoma kuhakikisha zinatenga ardhi kwa ajili ya watu wenye ulemavu na kusisitiza kuwa ardhi hiyo ni lazima iipimwe na kutolewa hatimiliki. Aidha ametaka ardhi hiyo itakayotengwa kwenye kila wilaya itumike kujengea ofisi za chama cha walemavu Tanzania Ngazi za wilaya na kufanyia miradi ya uzalishaji illi kujipatia kipato.
Vilevile Dr. Nchimbi alitoa Rai kwa chama cha walemavu Tanzania CHAWATA mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanaanzisha miradi ya ufugaji nyuki ambayo wataifanyia kwenye ardhi watakazopatiwa na wilaya.

Dr. Nchimbi aliyasema hayo jana alipokuwa akifungua mkutano Mkuu wa mwaka wa CHAWATA mkoa wa Dodoma ambapo aliwatia moyo walemavu kwa kuwaeleza kuwa miradi ya ufugaji nyuki katika mkoa wa Dodoma imeonesha kufanya vizuri na soko zuri lipo ndani na nje ya Nchi. Aidha, Alieleza kuwa ufugaji nyuki hauhitaji fedha nyingi na wala haumuhitaji mtu kwenda kushinda kwenye mradi kila siku akifanya kazi badala yake nyuki wenyewe ndio wanafanya kazi ya uzalishaji, hivyo mradi huu wa ufugaji nyuki utakuwa wa manufaa sana kwa watu wenye ulemavu.

Aliahidi serikali kutoa msaada wa usimamizi na utaalamu katika miradi hiyo ya nyuki ambapo ameagiza maafisa ustawi wa jamii mkoa na wilaya kusimamia miradi itakayoanzishwa na maafisa nyuki wa wilaya wahakikishe wanahudumia miradi hiyo upande wa utaalamu na amezitaka halmashauri za wilaya wahakikishe wanaweka mkundombinu ya usimamizi ikiwa ni pamoja na kugharamia gharama za wasimamizi wa hiyo miradi.Hiyo

Dr. Nchimbi alimaliza kwa kuwaasa CHAWATA kuwa mapato ya miradi hiyo ya nyuki yatumike kugharamia gharama za uendeshaji wa shughuli za CHAWATA ili walemavu waendeshe shughuli zao bila kutegemea kuomba misaada, vilevile mapato hayo yanaweza kutumika miradi mingine zaidi ya uzalishaji na hivyo kuwanyanua walemavu mkoaniDodoma.

Nae katibu wa CHAWATA mkoa wa Dodoma Ndg. John Mlabu akiwasilisha taarifa ya chama chake Ameeleza kuwa wanakumbana na changamoto nyingi zikiwemo ukosefu vyumba vya ofisi za wilayani, halmashauri nyingi hazitengi bajeti kwa ajili ya walemavu,  walemavu kutotengewa maeneo ya biashara kwenye maeneo yanayoainishwa kufanyia biashara na gharama za visaidizi mwendo (magongo, wheelchairs na tricycle) kuwa juu.

Nyingine ni bei kubwa za viwanja vinavyouzwa na mamlaka ya uendelezaji makao makuu CDA ambapo walemavu hawawezi kuzimudu na vilevile majengo mengi hasa maghorofa na baadhi ya ofisi nyeti hayajazingatia miundombinu ya watumiaji walemavu.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akiwasisitiza wanajumbe wa chama cha walemavu Tanzania CHAWATA mkoa wa Dodoma kuanzisha miradi ya ufugaji nyuki ili kujiongezea kipato wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa chama hiko uliofanyika jana mjini Dodoma.
Picha ya pamoja kati ya mkuu wa mkoa wa Dodoma  Dr. Rehema Nchimbi ( wapili kutoka kushoto waliochuchumaa) na wajnachama wa chama cha walemavu Tanzania (CHAWATA) Mkoa wa Dodoma muda mfupi baada ya mkuu huyo wa mkoa kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa chama hiko uliofanyika jana mjini Dodoma.

Saturday, January 4, 2014

CHADEMA KWAWAKA MOTO WANACHAMA WACHAPANA MAKONDE MAHAKAMANI.

adema dceb7
Vurugu za aina yake zimezuka katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam, baada ya watu wanaodhaniwa kuwa wanachama wa Chadema kumzomea aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho, Zitto Kabwe.
Vurugu hizo zilihusisha wafuasi wa chama hicho wanaomuunga mkono Zitto na wale wanaompinga, ambao walikuwa wamebeba mabango ya kumsifia na wengine wakiwa wamebeba ya kumkashifu.
Katika vurugu hizo, baadhi ya wanachama hao waliamua kufanya doria isiyo rasmi ndani ya mahakama hiyo ya kuwasaka watu waliodai kuwa ni mamluki, huku wakimkamata askari kanzu, kabla ya kumpiga ngumi na kumchania shati mtu mmoja wakidai kuwa alikuwa akiwarekodi kwa kutumia simu yake ya mkononi.
Tukio hilo la aina yake lilitokea jana asubuhi ambapo kundi la wanachama hao, huku baadhi wakiwa wamevaa nguo za kaki zinazotumiwa na chama hicho kufika katika mahakama hiyo kwa lengo la kusikiliza kesi ya pingamizi iliyofunguliwa na Zitto.
Mara baada ya kuwasili kwa Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini, huku akiwa ameongozana watu kadhaa wakiwamo wanasheria wake na mabaunsa, wanachama hao walianza kumzomea huku baadhi wakimwita fisadi.
Hali hiyo iliibua zogo katika eneo la mahakama hiyo, hali iliyowalazimu maofisa kadhaa wa polisi kuingilia kati kwa kuamua kumchukua Zitto na kumhifadhi kwenye chumba maalumu na kumtoa saa 6 mchana kesi yake ilipoanza kusikilizwa. Baadhi ya mabango ya kumkashifu yalisomeka; Zitto tulimpenda, CCM imempenda zaidi, Zitto rudisha fedha za CCM.
Yale yaliyomsifia yalisomeka; Zitto kama Mandela na Zitto ni Mkombozi.Baada ya kumalizika kusikilizwa kwa kesi hiyo, saa 12 jioni wanachama hao walianza kurushiana ngumi, hasa baada ya kuibuliwa kwa mabango yaliyosomeka 'Zitto kwanza Chadema baadaye'.
Awali hali hiyo ilimfanya Zitto kutaharuki, huku mabaunsa wake wakijihami na kuanza kumlinda.
Baada ya Zitto kuhifadhiwa baadhi ya wanachama hao ambao waliingia kwa kuandikishwa majina yao getini, walianza kuwasaka watu waliowahisi kuwa mamluki, ambapo walimnasa askari kanzu na kuanza kumzonga wakimuhoji anapeleleza nini katika eneo hilo.
"Hapa tunataka kujua wewe ni nani na unataka nini hapa, maana hatukuelewi kabisa kwa nini unakuja kusikiliza mazungumzo yetu, jitambulishe," alisisika mmoja wa wanachama hao akimhoji askari huyo huku akiwa amemkandamiza ukutani,
"Tunajua wewe ni askari kwa nini hujavaa sare leo? Kisha unajichanganya kwenye kundi letu."
Kesi hiyo ilimalizika saa 12 jioni ambapo Zitto alitolewa chini ya ulinzi mkali wa polisi kwa kupitia mlango wa nyuma wa mahakama hiyo na kuwaacha wafuasi hao wakionyeshana ubabKabla ya kuanza kwa kesi hiyo, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alimwomba Jaji John Utamwa kuendesha kesi hiyo kwa lugha ya Kiswahili kwa kuwa inagusa sehemu ya masilahi ya umma, jambo ambalo liliibua shangwe kwa wafuasi wa chama hicho waliokuwa wamefurika katika mahakama hiyo.
Hata hivyo baada ya kesi kuanza kuendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, Jaji Utamwa alilazimika kuikatiza, na kuwakemea wanachama wa Chadema baada ya sauti za kuguna kusikika wakati wakili wa Zitto, Albert Msando alipokuwa akiwasilisha hoja kuhusu msingi wa kesi hiyo.
" Nataka kuwakumbusha hapa mahakamani ni tofauti na sehemu nyingine sauti zinazosikika sizitaki, anayeona kwamba yanayozungumzwa hakubaliani nayo kama hawezi kunyamaza atoke nje vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa," alisema Jaji Utamwa.
Kundi la Wanachadema hao huku wengine wakiwa wamevalia sare zao waliwasili mahakamani hapo ili kusikiliza kesi ya pingamizi iliyofunguliwa na Kabwe akiiomba Mahakama iwazuie Bodi ya Wadhamini wa Chadema, Katibu Mkuu pamoja na Kamati Kuu ya Chadema jana kumjadili, kumchukulia hatua, uamuzi wowote wala kuhusu uanachama wake.
Msingi wa kesi
Juzi Zitto aliomba Mahakama hiyo kuzuia Kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kumjadili hadi rufaa yake aliyoikata kwenye Baraza Kuu la Chadema itakaposikilizwa na kuamuliwa na wazuiwe kumwingilia katika utekelezaji wa majukumu yake ya ubunge wa Kigoma Kaskazini .
Pia aliiomba Mahakama hiyo Kuu kumwamuru Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa ampatie nakala ya mashtaka na maelezo ya uamuzi uliofikiwa na Kamati Kuu Novemba 22, 2013 na kusababisha avuliwe nyadhifa zake ili aweze kupeleka rufaa yake Baraza Kuu la Chadema kupinga uamuzi huo

Thursday, January 2, 2014

ZITO KABWE AWEKA PINGAMIZI MAHAKAMANI JINA LAKE LISIJADILIWE KATIKA KIKAO CHA KAMATI KUU CHA CHADEMA.


Baada ya kuwepo kwa kila dalili za Mh.Zitto kabwe kutotendewa haki na Kikao cha Kesho cha kamati Kuu chadema.Zitto ameamua kuweka pingamizi la kukao hicho,kimahakama inawezekana na inaruhusiwa kuweka pingamizi ama kikao kisiwepo au wasikujadili kwenye kukao husika.
Slaa na mbowe wamekuwa akionesha dhamila ya wazi ya kutaka kumfukuza Zitto bila kufuata katiba ya Chama.
Awali Mwanasheria wa Zitto aliweka bayana kuwa Zitto alivuliwa nyadhifa zake CHADEMA bila kupewa nafasi ya Kuhojiwa,Mashitaka n.k kitu ambacho ni Ukiukwaji Mkubwa wa katiba.
Lakini pia siku za Karibuni Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amenukuliwa na Vyombo vya habari akisema hayupo tayari kuona Zitto anarejeshewa vyeo Ili hali Zitto amekata rufaa Baraza kuu la chama(Chombo cha juu kabisa cha Maamuzi) na akishinda vyeo anarudishiwa.

MAMA MZAZI WA IGP ERNEST MANGU AMTAKA MTOTO WAKE KUFANYA KAZI KWA UADILIFU.


mama 0053e
Mama Mzazi wa Mkuu wa Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu, Mwanaidi Msengi, amemsihi mwanawe kufanya kazi kwa bidii asimwangushe Rais Jakaya Kikwete ili asije kujutia kumpa nafasi hiyo.
Mwanaidi alisema licha ya furaha kubwa aliyonayo, anamuasa mtoto wake kuchapa kazi kwa bidii kama njia mojawapo ya shukurani kwa Rais Kikwete kwa kumteua akiwa mwenyeji wa kwanza kutoka Mkoa wa Singida kushika wadhifa huo nyeti.(HD)
"Hii ni heshima kubwa sana kwangu binafsi, ndugu zake, wakazi wa Kijiji cha Kihunadi na Mkoa wa Singida, kwa hiyo lengo langu ni kumwombea mtoto wangu Mangu asimwangushe Rais... Eee Baba (Mungu) msaidie mwanangu atimize wajibu wake ipasavyo ili Rais Kikwete siku moja aseme hakukosea kumpa Mangu ukuu wa polisi," alisema Mwanaidi.
Juzi ndugu, jamaa na marafiki walifanya hafla ndogo iliyoambatana na vifijo, nderemo na bashasha na wakazi wa Kijiji cha Kihunadi, Tarafa ya Ilongero, mkoani Singida, alikozaliwa IGP huyo huku wakidai sasa kijiji chao kitajulikana haraka ndani na nje ya Tanzania.
Walisema licha ya kujulikana, changamoto mbalimbali zinazokikabili kijiji hicho zitapatiwa ufumbuzi wa kudumu mapema iwezekanavyo.
Mwanaidi alisema Mangu alianza kumwonyesha mafanikio tangu Shule ya Msingi Kinyagigi, kwani alikuwa na bidii ya kujisomea mara kwa mara alishika nafasi ya kwanza au ya pili.
Kwa mujibu wa Mwanaidi, IGP Mangu ni mtoto wa pili kati ya saba aliowazaa.
"Mangu ni wa pili kati ya watoto wangu saba baada ya kuolewa na baba yao, Jumbe Omari Mangu aliyefariki Aprili 27, 1988. Jina la Jumbe linatokana na kupewa kazi ya ujumbe wa wakoloni wakati wa ujana wake," alisema.
Wenyeji wa kijiji hicho, walisema wamekuwa wakiamini Mangu atafika mbali kwa kushika nafasi za juu za uongozi, kutokana na uadilifu, uchapaji kazi, ukaribu wake na wananchi, uaminifu na uwazi.
Mwanaidi alisema Mangu alipofaulu kwenda sekondari alilazimika kuomba ng'ombe kwa mke mweza, ili akamuuze apate fedha za kugharimia masomo ya mtoto wake.
"Mke mwenzangu alimtoa ng'ombe wake, lakini Mangu alipomuuza kwenye mnada pale Singida mjini, aliibiwa fedha zote na alirudi nyumbani akilia sana," alisema.
Alisema baada ya hapo alimwambia mtoto wake kwamba, ataanza kutengeneza vyungu kwa kutumia udongo wa mfinyanzi ili kupata fedha za kugharimia masomo yake."Nashukuru Mangu alinielewa vizuri kwa sababu alishiriki kubeba kichwani vyungu hivyo wakati wa kuviuza hadi kichwa chake kilikaribia kuwa kipara. Nilibuni chanzo kingine cha mapato ambacho kilikuwa ni kukoroga na kuuza pombe za kienyeji," alisema. Inadaiwa baba yake, IGP Mangu alioa wanawake sita kwa nyakati tofauti, lengo likiwa ni kupata mtoto wa kiume. Wengi wa wake zake walikuwa wakizaa watoto wa kike.

Wednesday, January 1, 2014

BREAKING NEEEEWZZZ!!! WAZIRI WA FEDHA WILLIAM MGIMWA AFARIKI DUNIA


Habari zilizoufikia mtandao huu hivi punde zinasema kuwa aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dkt. William Mgimwa amefariki dunia  huko nchini Afrika ya Kusini alikokuwa amelazwa katika Hospitali ya Mediclinic Kloff. 

Habari zaidi kuhusu msiba huu zitawajia kdri zitakavyokuwa zikipatikana. Mungu ilaze roho ya marehemu, Dkt. Mgimwa mahala pema peponi, Amina.