Saturday, August 3, 2013

KARIBU LIVE KUTOKA NANE NANE MKOANI DODOMA.

Ofisa kilimo, uzalishaji na Mbegu wa Wilaya ya Chamwino  Aithan Chaula akimuelezea jambo Waziri wa Kilimo na Chakula Mhandisi Christopher Chiza katika viwanja vya nanenane alipotembelea banda hilo kabla ya kuzindua rasmi maonyesho hayo juzi.
Waziri Chiza akikaribishwa kuangalia kikundi cha ngoma kilichokuwa kikitoa burudani kwa wananchi waliokuwa wakisubili hotuba ya uzinduzi wa  maonyesho ya wakulima katika viwanja vya nanenane Nzuguni Dodoma.
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhandisi Christopher Chiza akikagua Bustani za mbogamboga na matunda za Taasisi ya Magereza zilizopo viwanja vya nanenanea Dodoma na aliongozana Kamishna wa Magereza anaeongoza Divisheni ya Urekebishaji Wafungwa Deonice Chamlesile na mkuu wa mkoa  Dr. Rehema Nchimbi 
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhandisi Christopher Chiza akiangalia tunda aina ya Bilinganya kwenye banda la wilaya ya chamwino alipotem,belea kabla ya kuzindua maonyesho ya wakulima nanenane yaliyoanza tarehe 1 na yanatarajia kuhitimishwa Agost 7 kutokana na sikukuu ya idd kuangukia nanenane.
Waziri wa Kilimo chakula na ushirika Mhandisi Christipher Chiza, Mwenyekti wa uandaaji ya maonyesho ya wakulima[TASO] Engrbert Moyo na Mtoto Nunu aliyeambatana na Waziri Chiza wakitembea katika viwanya vya Nanenane wakati wa Uzinduzi wa maadhimisho ya wakulima kitaifa yanayofanyika Dodoma

(PICHA NA JOHN BANDA)

Friday, August 2, 2013

WAZIRI MKUU WA THAILAND AONDOKA BONGO BAADA YA KUHITIMISHA ZIARA YAKE YA SIKU TATU NCHINI.


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Waziri Mkuu wa Thailand kwa maafisa waandamizi mbalimbali wa serikali wakati wa kumsindikiza mgeni huyo aliyehitimisha ziara yake rasmi ya siku tatu nchini mchana huu. Hapo akipeana mkono na Mkumbwa Ally wa Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa
 Akisalimiana na Dr Hamisi Mwinyimvua

 Akiagana na Kamanda wa Mkoa maalumu wa kipolisi wa Dar es salaam Suleiman Kova.PICHA NA IKULU

Thursday, August 1, 2013

SHIDA YA KUVUTA SIGARA,ANGALIA WAVUTA SIGARA WANAVYODHIBITIWA HUKO KENYA

Baadhi ya wavutaji wa sigara wakiwa katika chumba kimoja katijati ta  jiji la nairobi wakivuta sugara kutokana na nchi ya kenya kuweka msimamo na kusimamia sheria ya kutovuta sigara katika eneo lenye watu wengine wasiotumia sigara. jambo hilo humfanya mtu kutembea umbali mrefu kutafuta eneo hilo maalum kwa uvutaji wa sigara tofauti na nchi nyinginezo mnapishana tu na wavutaji tena wakikupulizia moshi usini.