Tuesday, March 5, 2013

BIBI WA MIAKA 67 AUWAWA AFRIKA KUSINI AKITAKA KUFUNGA NDOA NA KIJANA WA MIAKA 28



1
Jette-Jesse-600x349Polisi wa Afrika Kusini bado wanaendelea kuchunguza tukio la kutisha linalodaiwa kufanywa na kijana wa Kinigeria mwenye umri wa miaka 28 ambae anatuhumiwa kumuua bibi wa kizungu mwenye umri wa miaka 67 huko Johannesburg.
Bibi kizee Jette Jacobs ambae ni raia wa Australia alisafiri mpaka Johannesburg kwa lengo la kufunga ndoa na mwanaume anayempenda lakini siku mbili baada ya kukutana na mwanaume huyo, bibi huyo amekutwa amefariki kwenye mazingira ya kutatanisha kwenye jiji hilo lililo kwenye list ya majiji hatari kwa uhalifu duniani.
Johannesburg South Africa.
Johannesburg South Africa.
Jette alipokwenda Johannesburg lengo lake lilikua ni kukutana kwa mara ya kwanza na mwanaume ambae wamekua wakiwasiliana kupitia mtandao wa kijamii ambao hukutanisha watu wenye hitaji la kupata mpenzi/mke/mume ambapo aliingia kwenye mapenzi na Jesse Orowo Omokoh asiemjua miaka mitatu iliyopita.
Mwili wa bibi huyu mwenye watoto sita ulikutwa kwenye guest house miezi miwili baada ya kuwasili Afrika Kusini ambapo kwa muda waliofahamiana online, Jette alikua ameshatuma kiasi cha dola za Kimarekani laki mbili kwa Omokoh na mwanaume mwingine aitwae Isaac.
Pamoja na kupewa onyo na familia yake, Jette hakusikia chochote bali alitaka kwenda South Africa toka november 2012 ili akafunge ndoa na huyu mwanaume wa Kinigeria, kwenye guest house mwili wake ulipokutwa kuna baadhi ya vitu alivyokuwa navyo havijaonekana kama vile mikufu na pesa.
Binti wa mwisho wa bibi huyu amesema mwanaume huyu wa Nigeria alitaka kuhamia Australia ili akaishi na Bibi huyu lakini bibi aligoma na kumwambia anataka kwenda kuishi nae Nigeria.

Monday, March 4, 2013

MIGOGORO YA ARDHI NCHINI INAPOLETA BALAA

diwan akizingua hapatosh pande izzo ....
bibi huyu akiwa na bonge la bisu katika moja ya mikutano ya hadhara juu ya utatuzi wa ardhi hususan migogoro ya wakulima na wafugaji huko...........................hapa ukimzingua tu unae.

HII NDIO PATROL YA FFU JIJINI NAIROBI LEO

PARTOLS IN NAIROBI...NI KUBAYA,LETA SHIDA UJUE KACHUMBARI SIO MBOGA....... #FFU
PARTOLS IN NAIROBI...NI KUBAYA,LETA SHIDA UJUE KACHUMBARI SIO MBOGA....... #FFU

HUKO KENYA MCHAKATO BADO UNAENDELEA JAMANI CHEKI MSULULU WA WATU HAPA

KOCHA STARS KIM POULSEN ASHIRIKI NA KUMALIZA MBIO ZA KILIMANJARO MARATHON

Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) akimaliza mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon za Kilomita 21 zilizofanyika leo mjini Moshi. (Picha: Executive Solutions

AZAM FC YAIRARUA AL-NASRI YA SUDAN 5-0


TIMU ya Azam Fc, ya jijini Dar es Salaam, ambao ni wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho (CAF),jana tena imeeilambisha Al-Nasri ya Sudan jumla ya Ice Cream 5-0, katika mchezo wao wa marudiano uliochezwa leo katika Uwanja wa Juba, Sudan ya Kusini.
Katika mchezo wa awali uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Azam waliilaza timu hiyo kwa mabao 3-1, ambapo sasa Azam imefanikiwa kusonga mbele katika katika michuano hiyo kwa kuibanjua jumla ya mabao 8-1 timu hiyo

LIBOLO NOMA SANA NYIE KUMUUA SIMBA 5-0 SI MCHEZO

 Kikosi cha Simba, kilichoikabili timu ya Libolo ya Angola leo, ukumuondoa Haruna Moshi. Habari zilizoufikia mtandao huu hivi punde zinasema kuwa timu ya Simba imefungwa mabao 4-0 katika mchezo wake wa marudiano na timu ya Libolo ya Angola, katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa uliochezwa leo nje kidogo na mji wa Angola.

Bao la kwanza limefungwa katika kipindi cha kwanza na mabao matatu yakifungwa katika kipindi cha pili.
Hii ni moja ya actions ya mchezo wa timu hizo uliopita katika uwanja wa Taifa.