Sunday, February 3, 2013

MWENYEKITI WA CCM RAIS KIKWETE AONGOZA MATEMBEZI YA MSHIKAMANO YA MIAKA 36 YA CCM MJINI KIGOMA LEO

Mwenyekiti wa CCM Rais Janakaya Kikwete akiongoza matembezi ya maadhimisho ya miaka 36 ya CCM, leo asubuhi kutoka eneo la Mnarani hadi ofisi ya CCM mkoa wa Kigoma leo. Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Dk. Amani Kaborou, Mama Salma Kikwete, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (kulia)
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiongoza matembezi ya mshikamano ya Miaka 36 ya CCM, mjini Kigoma leo
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiongoza matembezi ya Mshikamano ya Maadhimisho ya Miaka 36 ya CCM mjini Kigoma leo
Matembezi hayo yakipita eneo la Burega, Barabara ya Kigoma-Ujiji
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akiwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM, Sadifa Abdalla na Mkuu wa wilaya ya Kigoma Jumanne Maneo

Friday, February 1, 2013

pinda-"saidieni WATOTO WANAOISHI KWENYE MAZINGIRA HATARISHI"

wpid-Prime-Minister-Mizengo-Pinda

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema kila Halmashauri hapa nchini ina wajibu wa kuhakikisha kuwa mipango inayowekwa inalenga kusadia watoto walio katika mazingira hatarishi. Ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Februari mosi, 2013) wakati

ruaha umefika?

100 4355 c3090

KUTEMBEA UCHI KWA WASICHANA SIKU HIZI NI KAWAIDA SANA HEBU ANGALIA HII LAANA


Hivi  sasa  jamii inalia  na mavazi ya  nusu  uchi.Lakini nadhani  baada  ya kitambo kifupi  dada  zetu  wataanza  kutembea  uchi......

Thamani  ya  mwanamke  imepungua  na maadili yamepotea.Kisa  na mkasa  ni  Utandawazi  huku  wengine wakisingizia  umasikini....

Kama tatizo  ni umasikini basi  ni  bora turudi kijijini  tukalime.... 

JENEZA LAKUTWA SOKONI JIJINI MWANZA.JE HUU NI USHIRIKINA?

maajabu haya jeneza lakutwa sokoni jijini mwanza katikati ya magunia ya viazi
hili ndilo jeneza ambalo wananchi wamelihusisha na imani za kishirikina
jeneza lilokutwa sokoni jijini mwanza likiwa pamoja na magunia ya viazi
huyu ndiye mhusika wa kulileta jeneza hilo na ni mweyekiti wa soko kuu jijini mwanza

KINANA ASHIRIKI KAZI ZA KIJAMII KIBONDO

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Kumwambo, Wilayani Kibondo, Jana, baada ya kushiriki ujenzi wa chumba cha darasa, ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambayo kilele chake kitafanyika  Februari 3, 2013 kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akishiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM tawi la Kijiji cha Bunyambo Wilayani Kibondo, Jana, ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambayo kilele chake kitafanyika  Februari 3, 2013 kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma. Wengine ni baadhi ya viongozi na wananchi aliofuatana nao kwenye msafara wake. 
 Baadhi ya wazee, watendaji na wajumbe wa mashina wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (hayupo pichani) alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Maendeleo wa Kibondo, Jana, ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambayo kilele chake kitafanyika  Februari 3, 2013 kwenye Uwanja wa Lake tanganyika mjini Kigoma.