Meya wa Manispaa ya Iringa Alex Kimbe mwenye koti la suti akitolewa
mahabusu kwenda mahakamani kusikiliza kesi ilitolewa ikimkabili ya
kutishia kuua kwa bastola
Meya kushoto akiwa chini ya ulinzi
MSTAHIKI meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Alex Kimbe (chadema)
amepandishwa mahakamani kwa kosa la kutishia kumuua katibu wa UV CCM
wilaya ya Iringa mjini Alphonce Myinga wakati wa zoezi la uchaguzi mdogo
wa udiwani kata ya Kitwiru.
Meya Kimbe alifikishwa mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya
Iringa John Mpitanjia leo majira ya saa 3 asubuhi na kusomewa shitaka
hilo la jinai kesi namba 189 /2017.
Akisoma shitaka hilo wakili wa jamhuri Allysniki Mwinyiheni alisema kuwa
Kimbe alitenda kosa hilo Novemba 26 mwaka huu katika eneo la Kitwiru
mjini Iringa kwa kumtishia kumuua kwa bastola Myinga .
Hata hivyo Kimbe alikana kosa hilo na kesi hiyo kuja tena mahakamani
hapo kwa ajili ya kutajwa Desemba 12 mwaka huu na meya huyo yuko nje kwa
dhamana baada ya mahakama kukubali kumpa dhamana .
Wakati huo huo makada watano wa Chadema jana walifikishwa mbele ya
hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama ya mkoa wa Iringa Richard Kachele
kwa makosa matatu likiwemo la unyang’anyi .
Wakili wa jamhuri alisema mahakamani hapo kuwa washitakiwa hao Martha
Robarth , Leonard Kulujila, Christopher Gerlad,Samweli Nyanda na Asau
Bwile kwa pamoja wanashitakiwa kwa makosa matatu ambayo ni kujeruhi,
Unyang’anyi wa kutumia nguvu na utekaji .
Kuwa tukio hilo walilifanya Novemba 19 mwaka huu eneo la Kitwiru kwa
kumteka Dikri Frank kada pamoja na kumteka walimpokonya simu yake ya
mkononi yenye thamani ya shilingi 100,000 pamoja na kadi ya CCM moja.
Washitakiwa hao ambao wanatetewa na wakili CHarzy Luoga walikana kosa
hilo na kunyimwa dhamana kutokana na kosa la unyang’anyi katika kesi
hiyo namba 190/2017 kutokuwa na dhamana .
Wakili wa washitakiwa hao aliiomba mahakama kuagiza wapelelezaji wa kesi
hiyo kufanya haraka kwani wateja wake wana maumivu na mmoja hawezi hata
kusimama baada ya kuumizwa na polisi wakati walipokamatwa .
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 12 mwaka huu itakapofikishwa tena
kwa ajili ya kutajwa na washitakiwa wote walirudishwa mahabusu