Mke wa Jaji John Ruhangisa, Marehemu Laetitia
Kokuhangisa Ruhangisa enzi za uhai wake.
Jaji John Ruhangisa
Jaji John Ruhangisa (wa pili kushoto), akiwa na watoto wake wakati wa ibada ya mazishi ya mke wake Laetitia Kokuhangisa Ruhangisa iliyofanyika nyumbani kwake katika Kijiji cha Ibwera mkoani Kagera leo jioni. Kutoka kulia ni mtoto wake wa kwanza Moreen, David na Fiona.
Mapadre 30 wa Kanisa Katoliki wakiwa kwenye ibada
hiyo ya mazishi.
Viongozi mbalimbali , majaji, watawa na wananchi
wakiwa kwenye ibada hiyo.
Watawa wakiwa kwenye ibada hiyo.
Waimbaji wa Kwaya ya Kanisa Katoliki Parokia ya Ibwera
nao walikuwepo kwenye ibada hiyo.
Watoto wa Kanisa Katoliki wanaoshiriki kuongoza ibada mbalimbali wakiwa kwenye ibada hiyo.
Watoto wa Kijiji cha Ibwera nao walijumuika katika
mazishi ya mama yao Kokuhengesa.
Jaji John Ruhangisa akimfariji mtoto wake David.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Bukoba, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Henry Mwaibambe akimpa pole mtoto wa marehemu, David John Ruhangisa.
Hii ndio nyumba ya milele ya mpendwa wetu mke wa Jaji John Ruhangisa, Marehemu Laetitia Kokuhangisa Ruhangisa alimo lala nje ya nyumba Kijijini Ibwera. Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake libarikiwe.
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu, Laetitia Kokuhangisa Ruhangisa wakielekea kaburini tayari kwa mazishi.
Jeneza likishushwa kaburini.
Jaji John Ruhangisa akiweka udongo kaburini wakati wa
mazishi ya mke wake. Kushoto ni shemeji yake Sizer.
Padre aliyeongoza ibada hiyo akiweka msalaba katika kaburi la Laetitia Kokuhangisa Ruhangisa.
Jaji John Ruhangisa akifarijiana na watoto wake aliowakumbatia, Moreen (kulia) na Fiona (kushoto. Hakika inahuzunisha.
Jaji John Ruhangisa na watoto wake wakiweka shada
la maua kaburini.
Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, Fr. James Rugemalira akisaini katika kitabu cha maombelezo.
Mdau Erick Kashasha naye alikuwa ni miongoni mwa waombolezaji waliosaini katika kitabu cha maombolezo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba akisaini katika kitabu cha maombolezo.(Imeandaliwa na mtandao a www. habari za jamii.com)
Dotto Mwaibale
SIMANZI na majonzi viligubika leo jioni katika mazishi ya mke wa Jaji John Ruhangisa, Marehemu Laetitia Kokuhangisa Ruhangisa aliyefariki kwa ajali ya gari jijini Arusha.
Mazishi hayo yaliyofanyika katika Kijiji cha Ibwera katika mkoani Bukoba.
Viongozi mbalimbali wa Serikali na vyama vya siasa, Majaji, dini na wageni waalikwa kutoka ndani na nje ya mkoa wa Bukoba walikuwa ni miongoni mwa watu waliohudhuria mazishi hayo.
Akizungumza katika mazishi hayo Rais wa Mahakama ya Afrika Mashariki, Dk. Emmanuel Ugirashebuja alisema kifo cha mke wa Jaji Ruhangisa kiliwashitua na kuwahunisha.
"Kifo cha mke wa mwenzetu kimetusikitisha sana kwani marehemu enzi za uhai wake tulikuwa tukijumuika naye kwa mambo mbalimbali kwa kweli tupepoteza mtu muhimu" alisema
Ugirashebuja alisema mafanikio yote aliyoanyo Jaji John Ruhangisa yametokana na maisha ya upendo aliyokuwa mke wake kwake ndio maana alipata fursa ya kufanya kazi kwa bidii kwa kuwa hakuwa na matatizo nyumbani kwake.
Mazishi hayo yalihudhuriwa na majaji kadhaa akiwemo Rais aliyepita wa Mahakama ya Afrika Mashariki, Jaji Nsekela, Jaji Rutakangwa aliye mwakilisha Jaji Mkuu wa Tanzania, Mwakilishi kutoka Halmshauri ya Meru
Mke wa Jaji Ruhangisa alipoteza maisha Oktoba 29 mwaka huu Tengeru mkoani Arusha wakati akitoka kazini baada ya Hiace aliyokuwa amepanda kugongwa na lori la mafuta.
Katika ajali hiyo watu 12 walipoteza maisha wakiwemo maofisa elimu watatu wa Halmshauri ya Meru